Kuhusu Mfumo wa Parokia Yetu

Mfumo wa Parokia yetu (MPY) ni mfumo wa kielektoniki unaoratibisha utunzaji na upatikanaji wa data (Taarifa) za parokia na hivyo kurahisisha usimamizi wa shughuli mbalimbali za parokia kwa kutunza data za parokia na kutoa taarifa mbalimbali kwa wakati zinapohitajika.

Parokia nyingi zimekuwa na changamoto ya kukosa mfumo mzuri wa kutunza kukmbukumbu na taarifa kwa usahihi. Changamoto hii imekuwa ikisababisha mahangaiko kwa viongozi, watendaji na waamini yakiwemo yafuatayo;


  • Kupotea kwa kumbukumbu / Taarifa muhimu.
  • Taarifa kutokupatikana kwa wakati.
  • Gharama kubwa za utunzaji wa data / Taarifa.
  • Usumbufu kwa waamini ambao wakati mwingine husubiri kwa muda mrefu kupata huduma.
  • Kusimama kwa kazi za parokia kwa sababu Padri au kiongozi au muhudumu amesafiri au anaumwa.
  • Kufanya kazi kubwa wakati wa kuandaa taarifa hivyo kuongeza uwezekano wa makosa kwenye taarifa.
  • kushindwa kupata taarifa sahihi nakupelekea kushindwa kufanya maamuzi sahihi.
  • Kazi ya kutafuta Taarifa kuwa ngumu.
  • Kupoteza muda mwingi kutafuta na kuandaa taarifa.
  • Waamini kulazimika kusafiri umbali mrefu kufuatilia taarifa zinazowahusu.
  • Maamuzi kuchukua muda mrefu kwa sababu ya kuchelewa kwa taarifa.
  • Kupata hasara mbalimbali kwa sababu ya kupotea kwa taarifa au kuwa na taarifa ambazo sio sahihi.
  • Kutoa huduma za kanisa kwa watu wasiostahili kwa sababu ya kutokuwa na taarifa sahihi.
  • Kukosewa, kupungua au kukosekana kabisa kwa taarifa za kiuongozi / kiutendaji za historia za miaka ya nyuma.

Changomoto hizo tajwa hapo juu husababisha usimamizi wa shughuli za kanisa kuwa mgumu.


MPY imetatua changamoto zote hizi ili kuongeza ufanisi na kasi ya huduma na maendeleo. MPY sasa inafanya haya:

  • Kutunza Taarifa kwa njia ya kielektroniki, kwa usalama mkubwa na kwa muda mrefu zaidi.
  • Kutoa taarifa mbalimbali za parokia kwa usahihi na kwa wakati.
  • Kupunguza gharama za kutunza Taarifa na kuondoa gharama mbalimbali zisizokuwa za lazima, na hivyo kupunguza gharama za usimamizi kwa ujumla.
  • Unakuwezesha kufanya maamuzi sahihi kwa sababu ya kuwa na taarifa sahihi.
  • Kuandaa taarifa kwa usahihi na urahisi zaidi.
  • Kutafuta na kupanga data kwa usahihi na uharaka zaidi.
  • Kusafirisha taarifa kwa haraka na wepesi kadiri yauhitaji.
  • Kuwa na kumbukumbu za miaka ya nyuma pasipo shaka, makosa wala usumbufu.
  • Kuongeza mapato ya Parokia kwa sababu ya uratibu mzuri na rafiki wa michango ya zaka, shukrani, Tegemeza parokia n.k.
  • Kumuwezesha Paroko / Padri, kiongozi, au muhusika yeyote kupata taarifa, kufanya maamuzi stahiki, au kutoa huduma inayohitajika hata usiku wa manane ikibidi, au hata akiwa safarini mbali ndani na nje ya nchi.
  • Kufanya maamuzi kwa wakati kwa sababu taarifa inapatikana kwa wakati.

MPY ni zao la Teknolojia, Teknolojia ni tunda la Sayansi, Sayansi ni matokeo ya Elimu na Elimu ni Paji la roho mtakatifu. MPY inabadilisha mfumo wa utendaji wa parokia kuendana na hali ya sasa ya sayansi na teknolojia ambayo roho mtakatifu anaendelea kuijalia dunia na yeye mwenyewe anaiboresha siku hadi siku, ili wanadamu tufanye vizuri zaidi katika kutimiza wajibu wetu wa kuitiisha dunia na kuyatatifuza malimwengu.

Tunakaribisha parokia mbalimbali kutumia MPY ambayo pia ina gharama nafuu kabisa.


Kama una Swali au Ushauri, Tafadhali wasiliana nasi, kwa Mawasiliano zaidi << Bofya hapa >> .